Romans 15:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo imekuwa nia yangu kuhubiri Injili pale ambapo Al-Masihi hajajulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Imekuwa shabaha yangu daima kuzihubiri Habari Njema katika sehemu ambako watu hawajawahi kusikia juu ya Kristo. Nafanya hivi kwa sababu sitaki kujenga katika kazi ambayo tayari mtu mwingine amekwisha kuianza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Al-Masihi amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikajitunukia, nisiipige hiyo mbiu njema mahali, Kristo alipokwisha kutangazwa, maana nisiujengee msingi wa mtu mwingine,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nayo nia moja niliyokuwa nayo ni kuhubiri tu Habari Njema fasi zote ambapo habari za Kristo zilipokuwa hazijasikilika bado. Nilikusudia vile kusudi nisijenge juu ya musingi uliowekwa na mutu mwingine,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine,