Romans 15:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi hadi huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana nataraji kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kusafirishwa nanyi, moyo wangu ushibe kwenu kidogo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo nitawatembelea nitakapoenda Hispania. Ndiyo, napanga kusafiri kwenda Hispania na natumaini kuwatembelea nikiwa njiani. Nitakaa kwa muda na kufurahi pamoja nanyi. Kisha natumaini mtanisaidia kuendelea na safari yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakati wowote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana natarajia kuwaona ninyi nikiwa katika safari, na kusafirishwa nanyi, baada ya kukaa kwenu kwa muda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nitawafikia hapo, nitakapokwenda Spania. Kwani natazamia kuonana nanyi, nitakapopita, nisindikizwe nanyi kwenda huko; lakini kwanza tupeane kikomo cha maneno na kufurahishana kitambo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana nataraji kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kusafirishwa nanyi, moyo wangu ushibe kwenu kidogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa hiyo nitawafikia nitakapokwenda Spania. Ninatumaini kupitia kule na kuonana nanyi, na kisha kufurahi kwanza pamoja nanyi kwa muda mufupi, ningetamani kupata musaada wenu kwa ajili ya safari ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.