Romans 15:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hata Al-Masihi hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe yalinipata mimi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hata Kristo hakuishi ili kijaribu kujifurahisha yeye mwenyewe. Kama Maandiko yanavyosema, “Matusi ambayo watu waliyatoa dhidi yako pia yalinifanya niteseke.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe yalinipata mimi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hata Al-Masihi hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe yalinipata mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani naye Kristo hakujipendeza mwenyewe; ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa: Masimango yao wanaokusimanga yameniguia mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana hata Kristo hakufanya mambo yanayomupendeza mwenyewe sawa vile ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Matusi wanayokutukana, yananiangukia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Kristo nae hakujipendeza nafsi yake; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu yalinipata mimi.