Romans 15:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu atoaye saburi na faraja awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Al-Masihi Isa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Subira na kuhimiza kote hutoka kwa Mungu. Na ninawaombea ili Mungu awasaidie muwe na nia ile ile ninyi kwa ninyi, kama ilivyo nia ya Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni ninyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Al-Masihi Isa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu mwenye uvumilivu na mwenye kuituliza mioyo ya watu awape, mioyo yenu nyote iwe mmoja tu, kama inavyowapasa walio wa Kristo Yesu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Mungu anayewapa watu nguvu ya kuvumilia na kufarijika awape kuwa na nia moja mukifuata mufano wa Kristo Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mungu mwenye uvumilivu na faraja awajalieni kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa namna ya Yesu Kristo;