Romans 15:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, haya ndiyo maneno yangu kwenu kwamba Kristo alifanyika mtumishi wa Wayahudi ili kuonesha kuwa Mungu amefanya yale aliyowaahidi baba zao wakuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nasema: Kristo aliwatumikia waliotahiriwa, ajulishe, ya kuwa Mungu ni mkweli, navyo viagio, baba walivyopewa, akavipatia nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana ninawaambia wazi kwamba Kristo alifanya utumishi kwa ajili ya Wayuda kwa kuhakikisha kuwa Mungu ni mwaminifu na kusudi atimize ahadi zile babu zetu walizopewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;