Romans 16:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mtu amesikia kuhusu utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu kwa Bwana, nami nafurahi sana juu ya hilo. Lakini ninataka muwe werevu kuhusu yaliyo mema na kutokujua lolote kuhusu yaliyo maovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya furaha yangu. Nawatakeni muwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani usikivu wenu umejulikana kwa watu wote; hivyo ninawafurahia. Lakini nataka, mwe werevu wa kweli, mambo yenu yawe mema, tena mwe wachanga wasioingia maovu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wanajua namna munavyomutii Bwana, na kwa sababu hii ninafurahi kwa ajili yenu. Lakini ninataka mukuwe wenye hekima kwa kutenda mema, na mukuwe safi mukijitenga na mambo mabaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana utii wenu umewafikilia watu wote; bassi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka mwe wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.