Romans 16:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naomba mpokeeni katika Bwana Isa ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nawaomba mmkaribishe kama yule aliye wa Bwana. Mkaribisheni kwa jinsi ambayo watu wa Mungu wanapaswa. Msaidieni kwa chochote atakachohitaji kutoka kwenu. Yeye amekuwa kiongozi anayeheshimika ambaye amewasaidia watu wengine wengi, pamoja na mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wo wote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naomba mpokeeni katika Bwana Isa ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lolote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, tena mmsaidie jambo lo lote, atakalopaswa nanyi. Kwani mwenyewe alitunza wengi, hata mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumupokee kwa ajili ya Bwana, kama vile watu wa Mungu wanavyopaswa kufanya. Mumusaidie katika kila jambo atakalohitaji toka kwenu, maana yeye amewasaidia watu wengi na hata mimi peke yangu vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu, kwa sababu yeye nae amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia na mimi pia.