Romans 16:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirishwa kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kweli hiyo sasa imeonyeshwa kwetu. Ilijulishwa kwa yale ambayo manabii waliandika katika Maandiko, kama Mungu wa milele alivyoagiza. Na sasa imejulikana kwa mataifa yote ili waweze kuamini na kumtii yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirisha kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirishwa kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirishwa kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yayo hayo yamefumbuliwa sasa na Maandiko ya Wafumbuaji kwa agizo lake Mungu, mwenye kuwapo kale na kale, wamizimu wote wafunzwe huo usikivu wa kumtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa yamefunuliwa na maandiko ya manabii kufuatana na amri ya Mungu wa milele, kusudi mataifa yote yapate kumwamini na kumutii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;