Romans 16:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Salimuni pia kundi la waumini wanaokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Al-Masihi huko jimbo la Asia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Vilevile, fikisheni salamu katika kanisa linalokusanyikia nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto. Alikuwa mtu wa kwanza kumfuata Kristo kule Asia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lisalimuni pia kanisa linalokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Kristo huko Asia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lisalimuni pia kundi la waumini linalokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Al-Masihi huko Asia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nisalimieni hata wateule waliomo nyumbani mwao! Nisalimieni mpenzi wangu Epeneto! Ndiye aliyeanza kumtegemea Kristo katika Asia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munisalimie vilevile kanisa linalokusanyika katika nyumba yao. Munisalimie mupendwa wangu Epeneto, anayekuwa mwamini wa kwanza wa Kristo katika jimbo la Azia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nisalimieni kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.