Romans 2:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fikirini kuhusu wasio Wahayudi ambao hawakukua wakiwa na sheria. Wanapotenda kama sheria inavyoamuru, wanakuwa kielelezo cha sheria, ijapokuwa hawana sheria iliyoandikwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mathalan: watu wa mataifa mengine hawana Sheria ya Mose; lakini kila wanapotimiza matakwa ya Sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha Sheria ingawa hawaijui Sheria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mathalani: watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Naam, wakati wa watu Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wamizimu wasiopata maonyo wakiyafanya mambo ya Maonyo wenyewe, basi, hao wasiopata maonyo mioyo yao ndiyo iliyokuwa maonyo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa mataifa hawana Sheria ya Musa. Lakini wanapofanya sawa inavyoamuriwa na Sheria ile kutokana na zamiri yao, wao ni Sheria kwa ajili yao wenyewe, ijapokuwa hawana Sheria ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe: