Romans 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wanaonesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanaonesha kuwa wanafahamu kilicho sahihi na kibaya, kama sheria inavyoamuru na dhamiri zao zinakubali. Lakini wakati mwingine mawazo yao huwaambia kuwa wamekosea au wamefanya sahihi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwenendo wao unaonyesha kwamba matakwa ya Sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao waionesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri zao zikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao wanaonyesha, ya kuwa kazi, Maonyo yanayoitaka, imeandikwa mioyoni mwao; nayo, wanayoyajua mioyoni, huwashuhudia, ndiyo mawazo ya mioyo yanayoinukiana, nayo mengine yanayokaniana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana wanaonyesha kwamba maagizo ya Sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Zamiri yao vilevile inawahukumu, na mawazo yao yenyewe yanawashitaki au yanawatetea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana;