Romans 2:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kupitia kwa Isa Al-Masihi, kama isemavyo Injili yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo itakavyokuwa siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu kupitia Yesu Kristo, sawasawa na Habari Njema ninayoihubiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Isa Al-Masihi, kama isemavyo Injili yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na Injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya yatajulikana siku ile, Mungu atakapompa Kristo Yesu kuyaumbua yaliyofichwa na watu. Huu ndio Utume mwema, niliopewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo ndiyo itakayotokea siku ile Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya watu kwa njia ya Yesu Kristo, kama vile Habari Njema yangu inavyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.