Romans 2:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kujigamba ati unayo sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja sheria unamdharau Mungu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe ujivuniaye Torati, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja Torati?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Unajivuna sana kwamba una sheria ya Mungu, lakini unamletea Mungu aibu kwa kuivunja sheria yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa kujigamba ati unayo Sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja Sheria unamdharau Mungu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kujigamba ati unayo sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja sheria unamdharau Mungu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kujigamba ati unayo sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja sheria unamdharau Mungu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Wewe, unayejivunia kwamba: Ninayo Maonyo, humbezi Mungu kwa kuyakosea Maonyo yake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unajisifu kwamba unajua Sheria, lakini unamuzarau Mungu kwa kuvunja Sheria!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wewe ujisifuye katika torati, kwa kuiasi torati wamvunjia Mungu heshima?