Romans 2:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii sheria. Lakini kama unaivunja sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii Torati, lakini kama unavunja Torati, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mnaifuata sheria, basi kutahiriwa kwenu kuna maana. Lakini mkiivunja sheria, mnakuwa kama watu ambao hawakutahiriwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii Sheria. Lakini kama unaivunja Sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii sheria. Lakini kama unaivunja sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutotahiriwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii sheria. Lakini kama unaivunja sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kutahiri kunafaa, kama unayashika Maonyo. Lakini ukiyakosea Maonyo, kutahiriwa kwako ni kwa bure, utakuwa tena kama mtu asiyetahiriwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutahiriwa kuna mafaa kama ukitii Sheria. Lakini usipotii Sheria, wewe unahesabiwa kama mutu asiyetahiriwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.