Romans 2:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja sheria, ingawaje unayo maandishi ya sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii sheria ingawa hawakutahiriwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii Torati watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana Torati ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnayo sheria na tohara, lakini mnaivunja sheria. Hivyo wale wasiotahiriwa katika miili yao, lakini bado wanaitii sheria, wataonesha kuwa mna hatia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja Sheria, ingawaje unayo maandishi ya Sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii Sheria ingawa hawakutahiriwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja sheria, ingawaje unayo maandishi ya sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii sheria ingawa hawakutahiriwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi Wayahudi, ambao mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu lakini mwaivunja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana Torati ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaivunja torati?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja sheria, ingawaje unayo maandishi ya sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii sheria ingawa hawakutahiriwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo mtu asiyetahiriwa aliye vivyo hivyo, alivyozaliwa, akiyatimiza Maonyo atakuumbua wewe uliye mwenye Maandiko na mwenye tohara, ukiwa unayakosea Maonyo
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu asiyetahiriwa kimwili, lakini anatii Sheria, atakuhukumu wewe unayevunja Sheria ijapokuwa unajua maandiko ya Sheria na umetahiriwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?