Romans 2:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho wa Mungu, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu kama huyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Myahudi halisi ni yule aliye Myahudi kwa ndani. Tohara halisi inafanywa moyoni. Ni kitu kinachofanywa na Roho, na hakifanyiki ili kufuata sheria iliyoandikwa. Na yeyote aliyetahiriwa moyoni kwa Roho hupata sifa kutoka kwa Mungu, siyo kutoka kwa watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya Sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani na tohara ya kweli ni jambo la rohoni, ni la kiroho, wala si la kimwili. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini aliye Myuda huko ndani kusikoonwa na watu, yeye ni Myuda. Nako kutahiriwa, kama ilivyoandikwa, siko; kwenye kweli ndiko kutahiriwa kwa moyo kunakowezekana kwa nguvu ya Roho; nako kutasifiwa, lakini siko kwa watu, ila kwa Mungu
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Muyuda wa kweli ni yule anayekuwa Muyuda kwa ndani, nako kutahiriwa kwa kweli ni kule Roho Mutakatifu anakofanya ndani ya moyo wa mutu, wala si kule kunakofanyika kwa njia ya maandiko ya Sheria. Mutu wa namna hii hapati sifa kutoka kwa watu lakini kutoka kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.