Romans 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza na watu wa mataifa mengine pia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Matatizo na mateso yatampata kila mmoja anayetenda uovu; kuanzia Wayahudi kwanza kisha wale wasio Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza na watu wa mataifa mengine pia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu Mataifa pia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza na watu wa mataifa mengine pia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maumivu na masongano yataupata moyo wa kila mtu anayefanya maovu, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mateso na taabu zitamupata kila mutu anayefanya mabaya: kwanza Wayuda, kisha watu wa mataifa mengine vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mateso na shidda juu ya killa roho ya mwana Adamu atendae uovu, kwanza Myahudi na Myunani pia: