Romans 3:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Makoo yao ni makaburi wazi; kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.” “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Maneno yao ni ya hatari kama kaburi lililo wazi. Wanatumia ndimi zao kwa kusema uongo.” “Maneno yao ni kama sumu ya nyoka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Makoo yao ni makaburi wazi; kwa ndimi zao hufanya udanganyifu.” “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Makoo yao ni makaburi wazi; kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.” “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira iko chini ya midomo yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makoo yao huwa makaburi yaliyo wazi, ndimi zao huzitumia uwongo tu, sumu ya pili imo midomoni mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vinywa vyao ni kama kaburi wazi, ndimi zao ni za kudanganya, ndani ya midomo yao munatoka sumu kali sawa ya nyoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Koo lao kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila, Sumu ya pili ni chini ya midomo yao.