Romans 3:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haki hii inayotoka kwa Mungu hupatikana kwa Isa Al-Masihi kwa wote wanaomwamini. Kwa maana hapo hakuna tofauti,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Uaminifu wa wema wa Mungu umedhihirishwa kwetu kupitia imani katika Yesu Kristo. Hufanya hivi kwa wote wanaomwamini Kristo. Kwa sababu kwa Mungu watu wote ni sawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Isa Al-Masihi kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wongofu wa Kimungu ndio huu: mwanzo ni kumtegemea Yesu Kristo, nao mwisho: wote wanaomtegemea huupata. Kwani hawapitani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kuhesabiwa haki na Mungu kunapatikana kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote wanaoamini, kwa maana hakuna tofauti yoyote kati yao,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.