Romans 3:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La, bali kwa ile sheria ya imani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, sisi Wayahudi tuna nini cha kujivunia? Hatuna kitu. Mungu amefunga mlango kuzuia nje kiburi cha Kiyahudi. Sheria gani husema hivyo? Sheria inayohimiza matendo? Hapana, ni sheria inayosisitiza imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza Sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, majivuno yako wapi? Yamefungiwa! Kwa nguvu ya maonyo gani? Ni yale yanayotaka matendo? Hapana, ni Maonyo yanayotaka kutegemewa tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sasa mutu ataweza kujivuna? Hapana! Kwa sababu gani? Kwa sababu anatii Sheria? Hapana. Lakini kwa sababu anamwamini Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ku wapi, bassi, kujisifu? Knmefungiwa mlango. Kwa sharia ya namna gani? Kwa sharia ya matendo? La! bali kwa sharia ya imani.