Romans 3:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani hiyo hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuna Mungu mmoja tu. Atawahesabia haki Wayahudi kwa imani yao, na atawahesabia haki wasio Wayahudi kwa imani yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu ni mmoja, naye atawakubali Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani hiyo hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani Mungu ni mmoja tu; waliotahiriwa huwapatia wongofu, wakiwa wanamtegemea; vilevile wasiotahiriwa huwapatia wongofu, wakiwa wanamtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu kuna Mungu mumoja tu. Na ni yeye atakayewahesabia Wayuda na watu wa mataifa mengine haki mbele yake kwa njia ya imani ya kila wamoja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.