Romans 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipewa ishara ya tohara kuwa muhuri wa haki aliyokuwa nayo kwa imani hata alipokuwa bado hajatahiriwa. Kusudi lilikuwa kumfanya baba wa wote waaminio pasipo kutahiriwa, ili wahesabiwe kuwa wenye haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ibrahimu alitahiriwa baadaye ili kuonesha kuwa Mungu amemkubali kuwa mwenye haki. Tohara yake ilikuwa uthibitisho kwamba Mungu alimhesabia haki kwa njia ya imani hata kabla ya kutahiriwa. Hivyo Ibrahimu ni baba wa wote wanaoamini lakini hawajatahiriwa. Kama Ibrahimu, wao pia wamekubaliwa na Mungu kuwa wenye haki kwa sababu ya imani yao tu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipewa ishara ya tohara kuwa muhuri wa haki aliyokuwa nayo kwa imani hata alipokuwa bado hajatahiriwa. Kusudi lilikuwa kumfanya baba wa wote wale waaminio pasipo kutahiriwa na ambao wamehesabiwa haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipewa ishara ya tohara kuwa muhuri wa haki aliyokuwa nayo kwa imani hata alipokuwa bado hajatahiriwa. Kusudi lilikuwa kumfanya baba wa wote wale waaminio pasipo kutahiriwa na ambao wamehesabiwa haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatahiriwa, apate kielekezo, kiwe kama muhuri ya wongofu uliotoka kwa kumtegemea Mungu, alipokuwa hajatahiriwa bado. Hivyo yeye ni baba yao wote watakaomtegmea Mungu wakiwa hawakutahiriwa; maana nao sharti wawaziwe kuwa wenye wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya pale alitahiriwa, na kutahiriwa kwake kulikuwa kitambulisho cha kuhakikisha ile haki Mungu aliyomuhesabia kwa njia ya imani yake. Hivi Abrahamu akakuwa baba wa watu wote wanaoamini, ijapokuwa hawatahiriwi, kusudi wao vilevile wahesabiwe haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;