Romans 4:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Ibrahimu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Halikuwepo tumaini kwamba Ibrahimu angepata watoto, lakini alimwamini Mungu na akaendelea kutumaini. Na ndiyo sababu akafanyika kuwa baba wa mataifa mengi. Kama Mungu alivyomwambia kuwa, “Utakuwa na wazaliwa wengi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazao wako watakuwa wengi kama nyota!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Abrahamu akaamini, akakuwa Baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Uzao wako utakuwa mwingi mno.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Ibrahimu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Uzao wako utakuwa mwingi mno.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo palipokuwa pasipo kingojeo cho chote, alifuliza kukitegemea kingojeo cha kwamba: Atakuwa baba ya mataifa mengi, kama ilivyosemwa: Hivyo ndivyo, wao wa uzao wako watakavyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abrahamu aliamini na kutumainia mambo ambayo yasingewezekana kutumainia na hivi akakuwa babu ya mataifa mengi, kufuatana na maneno haya Mungu aliyomwambia: “Hivi ndivyo wazao wako watakavyokuwa wengi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako.