Romans 4:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alikuwa mzee wa karibu miaka 100, lakini imani yake haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe, Sara, alikuwa tasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibrahimu hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri hali ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiri hali ya kufa ya tumbo la Sara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ibrahimu alikuwa na umri uliokaribia miaka 100, hivyo alikuwa amevuka umri wa kupata watoto. Pia, Sara hakuweza kuwa na watoto. Ibrahimu alilijua hili vizuri, lakini imani yake kwa Mungu haikudhoofika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alikuwa mzee wa karibu miaka mia moja, lakini imani yake haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe, Sara, alikuwa tasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alikuwa mzee wa karibu miaka 100, lakini imani yake haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe, Sara, alikuwa tasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abrahamu hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri juu ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiri juu ya ufu wa tumbo la Sara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibrahimu hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri juu ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiri juu ya ufu wa tumbo la Sara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia moja), na hali ya utasa wa tumbo lake Sara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alikuwa mzee wa karibu miaka 100, lakini imani yake haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe, Sara, alikuwa tasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kumtegemea Mungu hakukumpungukia napo hapo, alipouona mwili wake, ya kuwa umekufa; maana alikuwa wa miaka kama mia; wala hapo, alipomwona mama yetu Sara, ya kuwa mwili wake umekufa vilevile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye alikuwa na umri wa miaka karibu mia moja, lakini imani yake haikupunguka alipofikiri juu ya hali yake iliyokuwa kama ya mwenye kungojea tu lufu wala juu ya hali ya Sara aliyekuwa hawezi tena kuzaa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara.