Romans 4:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tumesema imani ya Ibrahimu ilihesabiwa kwake kuwa haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, baraka hii ni kwa ajili ya waliotahiriwa tu? Au pia ni kwa ajili ya wale wasiotahiriwa? Tumekwisha sema ya kwamba Ibrahimu alikubaliwa kuwa ni mwenye haki mbele za Mungu kutokana na imani yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tunasema, “Imani ya Abrahamu ilihesabiwa kwake kuwa haki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tunasema, “Imani ya Ibrahimu ilihesabiwa kwake kuwa haki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi je! Heri hiyo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa tunanena ya kwamba kwake Abrahamu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, wenye kushangiliwa hivyo ndio waliotahiriwa au wasiotahiriwa nao? Kwani twasema: Aburahamu aliwaziwa kuwa mwenye wongofu kwa kumtegemea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uheri huu si kwa watu wanaotahiriwa tu, lakini ni kwa watu wasiotahiriwa vilevile. Kwa maana tumekwisha kusema kwamba Abrahamu alihesabiwa kuwa mwenye haki kwa njia ya imani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.