Romans 5:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha Kristo ambaye alikuja baadaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Musa, mauti ilitawala watu wote, hata wale ambao hawakutenda dhambi kwa kuvunja amri, kama alivyofanya Adamu, aliye mfano wa yule atakayekuja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Musa, mauti ilitawala juu ya kila mtu. Adamu alikufa kwa sababu alitenda dhambi kwa kutokutii amri ya Mungu. Lakini hata wale ambao hawakutenda dhambi kwa njia hiyo hiyo walipaswa kufa. Hivyo mtu mmoja Adamu anaweza kufananishwa na Kristo, Yeye ambaye angekuja baadaye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha yule ambaye atakuja baadaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha Kristo ambaye alikuja baadaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Mose, mauti ilitawala watu wote hata wale ambao hawakuvunja amri kama alivyofanya Adamu, ambaye alikuwa mfano wa yule atakayekuja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Musa, mauti ilitawala watu wote, hata wale ambao hawakutenda dhambi kwa kuvunja amri, kama alivyofanya Adamu, ambaye alikuwa mfano wa yule atakayekuja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha Kristo ambaye alikuja baadaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tangu Adamu mpaka Mose kifo kilishika ufalme hata kwao wale wasiokosa, kama Adamu alivyokosa kwa kubeza agizo. Naye ni mfano wake yeye aliyetazamiwa, atokee siku za halafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kifo kilitawala tangia wakati wa Adamu mpaka wakati wa Musa, hata juu ya wale wasiofanya zambi kwa kuvunja amri, sawa vile Adamu alivyofanya. Naye ni mufano wa yule aliyengojewa kuja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hatta wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakaekuja.