Romans 5:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja lilileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo dhambi hiyo moja ya Adamu ilileta adhabu ya kifo kwa watu wote. Lakini kwa njia hiyo hiyo, Kristo alifanya kitu chema zaidi kilichowezesha watu kufanyika wenye haki mbele za Mungu. Na hicho huwaletea uzima wa kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kimoja kiadilifu kinawapa uhuru na uzima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja kulileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja lilileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, ni hivi: Anguko la mmoja liliwapatia watu wote maangamizo, vivyo hivyo wongofu wa mmoja uliwapatia watu wote wongofu unaowapa uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kama vile kosa la mutu mumoja limewaletea watu wote azabu, ni hivi vilevile tendo la haki la mutu mumoja limewaweka huru na kuwapa uzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.