Romans 6:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, kwa kuwa alikufa — mara moja tu — dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu; lakini uzima alio nao anamwishia Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, Kristo alipokufa, alikufa ili aishinde nguvu ya dhambi mara moja, na siyo mara nyingine tena. Sasa anao uzima mpya, na uzima wake huo upo kwa nguvu za Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo, kwa kuwa alikufa—mara moja tu—dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, kwa kuwa alikufa — mara moja tu — dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, kwa kuwa alikufa – mara moja tu – dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivyo, alivyokufa, aliyafia makosa na kuyashinda papo hapo; lakini hivyo, anavyoishi, anaishi, amtumikie Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuelekea jambo la kufa kwake, alikufa mara moja tu kwa ajili ya zambi; lakini kuelekea maisha yake, sasa anaishi kwa ajili ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi marra moja; lakini kule kuishi kwake, amwishia Mungu.