Romans 6:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnajua kwamba mkijitolea nyinyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo — au watumwa wa dhambi na matokeo yake ni kifo, au wa utii na matokeo yake ni kufanywa kuwa waadilifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu yeyote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii? Iwe ni watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakika mnajua kuwa unakuwa mtumwa wa jambo lolote unaojitoa kulifanya. Chochote au yeyote unayemtii atakuwa bwana wako. Unaweza kufuata dhambi, au kumtii Mungu. Kufuata dhambi kunaleta kifo cha kiroho, lakini kumtii Mungu kunakufanya uhesabiwe na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo—au watumwa wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnajua kwamba mkijitolea nyinyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo — au watumwa wa dhambi na matokeo yake ni kifo, au wa utii na matokeo yake ni kufanywa kuwa waadilifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu ye yote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu yeyote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, iwe ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au iwe ni utumishi wa utii uletao haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnajua kwamba mkijitolea nyinyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo – au watumwa wa dhambi na matokeo yake ni kifo, au wa utii na matokeo yake ni kufanywa kuwa waadilifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hamjui, vilivyo? Ni hivi: mnapojitoa wenyewe kumtumikia mtu kitumwa na kumtii, basi, mmekwisha kuwa watumwa wake yeye, mnayemtii. Ikiwa ni wa ukosaji, mnakwenda kufa; ikiwa ni wa wito, mnakwenda kupata wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajua hakika kwamba mukijitoa wenyewe kwa mutu fulani kuwa watumwa wake na kulazimishwa kumutii, munakuwa kweli watumwa wa yule munayemutii. Ikiwa ni utumwa wa zambi, mwisho wake ni kifo; ikiwa ni kumutii Mungu, mwisho wake ni maisha ya haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki.