Romans 6:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini — namshukuru Mungu — mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu apewe shukrani kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo zamani mlikuwa watumwa wa dhambi na dhambi iliwatawala. Lakini ashukuriwe Mungu, mlitii kwa hiyari mafundisho yote aliyowaelekeza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini—namshukuru Mungu—mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini — namshukuru Mungu — mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini – namshukuru Mungu – mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mungu atolewe shukrani, kwa sababu ninyi mliokuwa watumwa wa ukosaji mmegeuzwa mioyo, mkaja kuyatii mafundisho, kama mlivyoyapata!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini asante kwa Mungu, kwa maana ninyi muliokuwa zamani watumwa wa zambi mumetii sasa kwa moyo wenu wote kanuni za mafundisho muliyopewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;