Romans 6:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uhai wa milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini sasa mko huru dhidi ya dhambi. Mmekuwa watumwa wa Mungu, na mnaishi kwa ajili ya Mungu tu. Hili litawaletea uzima wa milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sasa, mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uzima wa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uhai wa milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uhai wa milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa kwa kuwa mmekwisha kukombolewa katika utumwa wa ukosaji, mkawa watumwa wake Mungu, mnayo mapato yenu kwa kujifikisha penye kutakaswa, tena mwisho mtapata uzima wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa kufuatana na vile mumewekwa huru toka utawala wa zambi na kugeuka watumwa wa Mungu, munapata faida ya kuishi katika utakatifu na kwa mwisho kupewa uzima wa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele.