Romans 7:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu zangu, sasa ninasema na wale wanaoijua Torati: Je, hamjui kwamba Torati ina mamlaka juu ya mtu wakati akiwa hai tu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, ninyi nyote mnailewa sheria ya Musa. Hivyo kwa hakika mnafahamu kuwa sheria huwatawala watu wanapokuwa hai tu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua Sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu zangu (sasa ninasema na wale wanaoijua sheria.) Je, hamjui ya kwamba sheria ina mamlaka tu juu ya mtu wakati akiwa hai?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu zangu (sasa ninasema na wale wanaoijua Torati), je, hamjui ya kwamba Torati ina mamlaka tu juu ya mtu wakati akiwa hai?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na niseme nanyi, kwa kuwa mnayatambua Maonyo: Hamjui, ndugu: Maonyo humshika mtu siku zote za maisha yake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, munajua uhakika juu ya maneno haya nitakayowaambia, kwa maana ninyi ni watu wanaoelewa Sheria vizuri: Sheria haina mamlaka juu ya mutu isipokuwa tu wakati angali muzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HAMJUI, ndugu (maana nasema nao waijuao sharia), ya kuwa torati humtawala mtu maadam yu hayi.