Romans 7:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mathalani: Mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuwa hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka sheria ya ndoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni kama ambavyo sheria kuhusu ndoa inavyosema: ni lazima mwanamke abaki katika ndoa mume wake akiwa hai. Lakini mume wake akifa, atakuwa amewekwa huru kutoka katika sheria ya ndoa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mathalan: mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuw hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mathalani: Mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuwa hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka katika sheria ya ndoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka sheria ya ndoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali yule mume akifa, amefunguliwa ile sheria ya mume.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mathalani: Mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuwa hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mwanamke aliye na mume siku za kuishi kwake mumewe ana mwiko kwa ajili ya Maonyo; lakini nguvu ya hayo Maonyo hukoma, mumewe anapokufa, hana mwiko tena wa mwanamume mwingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mufano, mwanamuke aliyeolewa anafungwa na Sheria katika maisha yake na mume wake wakati mume wake angali muzima. Lakini kama mume wake akikufa, yeye anakuwa huru kufuatana na Sheria ile iliyomufunga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana mwauamke aliye na mume amefungwa na sharia kwa yule mume maadam yu hayi: bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sharia ya mume.