Romans 7:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nimegundua kanuni hii: Ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo naiona Torati ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo nimejifunza hivi kuhusu sheria: Ninapotaka kutenda mema ambayo sheria inaamrisha, uovu unakuwa hapo hapo pamoja nami.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo naiona Torati ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nimegundua kanuni hii: Ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo mimi ninayetaka kukifanya kilicho kizuri, ninaona nguvu ngeni kwangu inayonishurutisha kukifanya kilicho kiovu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ninatambua kanuni hii: wakati ninapotaka kufanya jambo jema, mara moja ninavutwa kufanya jambo baya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi nimeona sharia hii ya kuwa nipendapo kutenda lililo jema, liapo lililo baya ni karibu nami.