Romans 7:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shukrani kwa Mungu afanyaye hivyo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: Mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu ninaitumikia sheria ya dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Namshukuru Mungu anayeniokoa kupitia kwa Isa Al-Masihi Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa Torati ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Namshukuru Mungu kwa wokovu wake kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo katika ufahamu wangu mimi ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika udhaifu wangu wa kibinadamu mimi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shukrani kwa Mungu afanyaye hivyo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu ninaitumikia sheria ya dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Isa Al-Masihi Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa Torati ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shukrani kwa Mungu afanyaye hivyo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: Mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu ninaitumikia sheria ya dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu atolewe shukrani kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Basi, kwa akili zangu mimi mwenyewe nayatumikia kitumwa Maonyo yake Mungu, lakini mwilini ni mtumwa wa maonyo ya ukosaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Basi hivi kwa upande mumoja ninatumikia sheria ya Mungu kwa akili yangu, lakini kwa upande mwingine ninatumikia sheria ya zambi kwa hali yangu ya kimwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi.