Romans 7:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Iwapo ataolewa na mwanaume mwingine, mume wake akiwa angali hai, sheria inasema kuwa ana hatia ya uzinzi. Lakini mumewe akifa, atakuwa amewekwa huru kutoka katika sheria ya ndoa. Hivyo akiolewa na mwanaume mwingine baada ya mumewe kufa, hatakuwa na hatia ya uzinzi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakati mumewe awapo hai, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za kuishi kwake mumewe, yeye akiwa wa mume mwingine, huitwa mzinzi. Lakini mumewe anapokufa, amefunguliwa na Maonyo, asiwe tena mzinzi akiwa wa mume mwingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kama akiolewa na mutu mwingine wakati mume wake angali muzima, atahesabiwa kuwa muzinzi. Lakini kama mume wake akikufa, yeye anakuwa huru toka Sheria ile iliyomufunga na hata akiolewa na mutu mwingine hatahesabiwa kuwa muzinzi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakati awapo hayi mume wake, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Bali mume wake akifa, amekuwa huru, hafungwi na sharia hiyo, hatta yeye si mzinzi, ajapokuwa na mume mwingine.