Romans 7:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: Nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia Torati kupitia kwa mwili wa Al-Masihi, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa njia hiyo hiyo, kaka na dada zangu, mliwekwa huru kutoka katika sheria utu wenu wa zamani ulipokufa pamoja na Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye yule aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Sote ni mali ya Kristo ili tutumike kwa ajili ya huduma kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hali kadhalika ninyi ndugu zangu: ninyi pia mmekufa kuhusu Sheria kwa kuwa ninyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuka kutoka kwa wafu, ili kwamba tupate kuzaa matunda kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia Torati kwa njia ya mwili wa Al-Masihi, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: Nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu zangu, hapo Kristo alipokufa, mliuawa nanyi, mkayafia Maonyo; kwa hiyo mmefunguliwa nanyi kuwa wa mwingine, maana ni wa yule aliyefufuliwa katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nanyi wandugu zangu, ni hivi inavyokuwa kwa ngambo yenu. Kufuatana na maneno ya Sheria, ninyi vilevile mumekufa, kwa maana muliungana na mwili wa Kristo. Na sasa munakuwa wa mutu mwingine, ndiye yule aliyefufuka, kusudi tupate kufanya matendo yanayofaa katika kazi ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda.