Romans 7:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini dhambi ilipata nafasi katika amri, nayo ikazaa kila aina ya tamaa ndani yangu. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na dhambi kwa kutumia amri hiyo, ikanifanya nitamani kila kitu kisichokuwa changu. Hivyo dhambi ilikuja kwangu kutokana na amri hiyo. Lakini bila sheria, dhambi imekufa na haina nguvu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila Sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ukosaji ulianzia hapohapo penye agizo hilo, ukakuza moyoni tamaa yo yote, ukaitia nguvu; kwani pasipo Maonyo ukosaji ni mfu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutokana na amri, zambi ilipata njia hata kuamusha kila namna ya tamaa ndani yangu. Kwa maana pasipo Sheria zambi ingekuwa kama mufu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanza ndani yangu killa namna ya tamaa. Kwa maana dhambi hila sharia ni kifu.