Romans 8:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Al-Masihi Isa kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kupitia kwa Roho wake Mtakatifu akaaye ndani yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu. Na ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu, ataifanya hai tena miili yenu inayokufa. Ndiyo, Mungu ndiye aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu, naye atawafufua ninyi na kuwapa uzima kupitia Roho wake anayeishi ndani yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi ikiwa Roho wa Mwenyezi Mungu aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Al-Masihi Isa kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Roho yake yule aliyemfufua Yesu katika wafu ikiwakalia mioyoni, yuyu huyu aliyemfufua Yesu Kristo katika wafu atairudisha uzimani hata miili yenu, itakapokwisha kufa; atayafanya kwa nguvu ya Roho yake inayowakalia mioyoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama Roho wa Mungu aliyemufufua Yesu anakaa ndani yenu, basi huyo aliyemufufua Kristo ataupatia mwili wenu unaokuwa wa kufa uzima kwa njia ya Roho wake anayekaa ndani yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.