Romans 8:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo, ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Al-Masihi, naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nasi kwa kuwa ni watoto wa Mungu, basi sisi ni warithi, warithi wa Mungu na warithi pamoja na Kristo. Mungu atatupa yale yote aliyompa Kristo. Sisi tunaoteseka sasa kama Kristo alivyoteseka tutashiriki katika utukufu wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo, ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo, ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Al-Masihi, naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tukiwa watoto, basi, tunakuwa hata warithi, maana warithi wake Mungu watakaopata urithi pamoja na Kristo; tukiwa tunateswa pamoja naye tutapata hata kutukuzwa pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama sisi ni watoto, basi tutakuwa na sehemu katika urizi ule Mungu aliowaahidi watu wake, na tutashiriki pamoja na Kristo katika urizi ule; kwa maana kama tukiteswa pamoja naye tutatukuzwa pamoja naye vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.