Romans 8:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho wa Mungu, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani ukombozi wa miili yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siyo uumbaji tu, bali sisi pia tumekuwa tukingoja kwa kuugua na uchungu ndani yetu. Tunaye Roho kama sehemu ya kwanza ya ahadi ya Mungu. Kwa hiyo tunamngoja Mungu amalize kutufanya sisi watoto wake yeye mwenyewe. Nina maana kuwa tunasubiri kuwekwa huru kwa miili yetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukitazamia kufanywa watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena sivyo hivyo tu, ila na sisi wenyewe tuliokwisha pata malimbuko ya Roho twapiga kite ndani mioyoni tukichungulia kuwa wana, kwani ndipo, miili yetu nayo itakapokombolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na si viumbe hivi tu; hata sisi tuliokwisha kuwa na Roho wa Mungu kama sehemu ya kwanza ya zawadi Mungu atakazotoa, tunaugua vilevile ndani yetu, tukingojea kukubaliwa na Mungu kuwa watoto wake, maana yake kukombolewa kwa kimwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala si hivyo tu, illa na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho tunaugua katika nafsi zetu, tukitazamia kufanywa wana, ukombozi wa mwili wetu.