Romans 8:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana, basi hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alicho nacho tayari?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuliokolewa ili tuwe na tumaini hili. Ikiwa tunaweza kuona kile tunachokisubiri, basi hilo siyo tumaini la kweli. Watu hawatumaini kitu ambacho tayari wanacho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa; lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho tayari?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alicho nacho tayari?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini; lakini kitu kilichotumainiwa kikionekana, hakiwi tumaini tena. Kwa maana ni nani anayekitumainia kile akionacho?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kwani kingojeo, ambacho tuliokolewa, tuwe nacho, hicho ndicho; lakini kingojeo kinachoonekana machoni sicho kingojeo. kwani hilo, mtu analoliona, analingojeaje?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana tumeokolewa, lakini ni kwa tumaini. Mutu akiona kitu anachokitumainia, hilo si tumaini tena, kwa maana nani anayeweza kuendelea kutumainia kitu anachokiona?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana tuliokolewa kwa kutumaini; lakini kitu kilichotumainiwa kikionekana hakuna kutumaini tena. Kwa maana kile akionacho mtu, ya nini kukitumaini?