Romans 8:31 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo tuseme nini juu ya hili? Ikiwa Mungu yuko kwa ajili yetu, hakuna anayeweza kuwa kinyume nasi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote tuyasemeje? Mungu akiwa upande wetu, yuko nani atakayetushinda?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kufuatana na mambo hayo, tuseme nini zaidi? Mungu akiwa upande wetu, ni nani anayeweza kupingana nasi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, na tuseme nini baada ya hayo? Mungu akiwa upande wetu, nani aliye juu yetu?