Romans 8:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye alimwacha mwanae ateswe kwa ajili yetu. Mungu alimtoa Mwanaye kwa ajili yetu sisi sote. Sasa kwa kuwa tu wa Kristo, hakika Mungu atatupa mambo mengine yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu hakumhurumia hata mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje pia kutupa chochote kingine pamoja naye?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakumwonea Mwana wake mwenyewe uchungu, ila alimtoa kwa ajili yetu sisi sote; kwa hiyo asitupatie sisi magawio yote kwake yeye?*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye hakumwacha Mwana wake wa pekee, lakini alimutoa kwa ajili yetu sisi wote. Namna gani atakosa kutupatia vilevile vitu vyote kwa njia ya mwana wake?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?