Romans 8:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili haki ipatikanayo kwa Torati itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alifanya hivi ili tuweze kuishi kama sheria inavyotaka. Sasa tunaweza kuishi hivyo kwa kumfuata Roho na si kwa jinsi ya udhaifu wa kibinadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya Sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili kwamba haki ipatikanayo kwa Torati itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wongofu unaotakwa na yale Maonyo utimilizike mioyoni mwetu sisi, tusioendelea kimtu, ila Kiroho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifanya vile kusudi maagizo ya haki ya Sheria yapate kutimizwa ndani yetu sisi tunaoishi kufuatana na uongozi wa Roho wa Mungu, lakini si kufuatana na hali yetu ya kimwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.