Romans 8:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ambaye hana Roho wa Al-Masihi, huyo si wa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninyi hamtawaliwi na udhaifu wenu wa kibinadamu, bali mnatawaliwa na Roho, ikiwa Roho huyo wa Mungu anakaa ndani yenu. Na mtu yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ninyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mwenyezi Mungu anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Al-Masihi, yeye si wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi ham wa kimtu, ila wa Kiroho, kama Roho ya Mungu inawakalia mioyoni; lakini asiye na Roho ya Kristo huyo si wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi sasa hamutawaliwi na hali yenu zaifu ya kimwili, lakini munatawaliwa na Roho Mutakatifu, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Na mutu yeyote asiyekuwa na Roho wa Kristo ndani yake, yeye si mutu wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.