Romans 9:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, kabla ya kuzaliwa wana hao mapacha, Mungu alimwambia Rebeka, “Mwana mkubwa atamtumikia mdogo.” Hii ilikuwa kabla wavulana hawa hawajatenda jambo lolote jema au baya. Mungu alisema hivi kabla hawajazaliwa ili kwamba mvulana ambaye Mungu alimtaka atachaguliwa kutokana na mpango wa Mungu mwenyewe. Mvulana huyu alichaguliwa kwa sababu ndiye ambaye Mungu alitaka kumwita, si kwa sababu ya jambo lolote walilofanya wavulana hao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lo lote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hapo, watoto walipokuwa hawajazaliwa, wala hawajafanya mema au maovu, hapo ndipo, Mungu alipowachagulia kwa hivyo, alivyowawekea kale, viwepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wale walipokuwa hawajazaliwa bado, wala hawajatenda jambo lolote zuri au baya, Mungu alimwambia Rebeka hivi juu yao: “Mukubwa atamutumikia mudogo.” Alisema vile kwa kutimiza mupango wake unaotokana na uchaguzi wake usiofuatana na matendo ya watu, lakini mwito wake kwao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,