Romans 9:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeye aliyefinyanga chungu anaweza kufinyanga kitu chochote anachotaka. Anautumia udongo ule ule wa mfinyanzi kufinyanga vitu mbalimbali. Anaweza kufinyanga kitu kimoja kwa makusudi maalumu na kingine kwa matumizi ya kila siku.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka katika bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfinyanzi haufanyishi udongo, kama anavyotaka? Donge lililo moja upande mmoja haliumbi kuwa chombo kizuri, nao upande mwingine kuwa kibaya?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufinyanzi anaweza kufanya sawa vile anavyotaka na udongo. Toka donge moja la udongo anaweza kutengeneza chombo kimoja cha heshima na kingine cha matumizi ya kawaida.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
An mfinyangi je! bana nguvu juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kufanya chombo kimoja, kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?