Romans 9:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alingoja kwa uvumilivu ili aweze kuutangaza utajiri wa utukufu wake kwa watu aliowachagua wapokee rehema zake. Mungu alikwisha waandaa kuushiriki utukufu wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha anataka kuutambulisha hata wingi wa utukufu wake kwao walio vyombo vitakavyo huruma, ndio, aliowapatia utukufu kale;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile alitaka kuonyesha uwingi wa utukufu wake kwa wale aliowasikilia huruma; wale ambao alitayarisha tangu zamani kwa kuwatukuzisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu,