Romans 9:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama, nitaweka huko Siyoni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Lakini atakayemwamini hataaibishwa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ilivyoandikwa: “Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu na mwamba wa kuwaangusha. Yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama ilivyoandikwa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maandiko yanazungumza kuhusu jiwe hilo: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni litakalowafanya watu wajikwae. Ni mwamba utakaowaangusha watu. Lakini yeyote atakayemtumaini yeye hataaibika kamwe.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama! Naweka huko Sioni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama, nitaweka huko Siyoni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Lakini atakayemwamini hataaibishwa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ilivyoandikwa: “Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza na mwamba wa kuwaangusha, ye yote atakayemwamini hataaibika kamwe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ilivyoandikwa: “Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu na mwamba wa kuwaangusha. Yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama, nitaweka huko Siyoni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Lakini atakayemwamini hataaibishwa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama ilivyoandikwa: Tazama, naweka humo Sioni jiwe la kujigongea na mwamba wa kujikwalia. Naye alitegemeaye hatatwezeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Angalia, ninaweka jiwe la kukwalisha katika Sayuni nalo ni la kuangusha. Lakini yule anayemwamini hatapata haya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama ilivyoandikwa, Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao: Na killa amwaminiye hataaibishwa.